Majambazi wawili wauawa Kigoma
Majambazi wawili wameuwawa mkoani Kigoma na mwingine kutoweka kusikojulikana baada ya majibizano ya risasi na jeshi la polisi wakati walipojaribu kuvamia soko la Kijiji cha Bukirilo lililopo wilayani Kakonko mkoani humo.