Miradi italeta tija kwa wananchi - Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kusimamia ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi inayojengwa katika maeneo yote nchini yakiwemo ya vijijini ili kuhakikisha inaleta tija na kuwawezesha wananchi kupata huduma bora kwa wakati.