"Ongezeko la wageni limeleta somo kubwa" - Waziri
Waziri wa Maliasili Balozi Dkt.Pindi Chana, amewaagiza viongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na TANAPA kuimarisha vikosi vya ujenzi ili vifanye ukarabati wa mara kwa mara wa miundombinu ya barabara na kushughulikia kwa haraka changamoto za kuharibika kwa miundombinu.