Auawa baada ya kuiba milioni 19 na vocha
Mtu mmoja anayedhaniwa kuwa ni jambazi, ameuawa kwa risasi na jeshi la polisi, baada ya yeye na wenzake watatu kuiba pesa zaidi ya shilingi milioni 19 na vocha za simu za mkononi, kutoka katika duka la mfanyabiashara Musa Maduhu wa kijiji cha Nemba, wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.