Kijiji cha Msomera kuwa shamba darasa la uchumi
Serikali imesema Kijiji cha Msomera kilichopo Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga kinawekewa mipango maalum ya kuwa shamba darasa la uchumi wa mifugo ambapo kwa kuanzia itaweka kambi hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha upandishaji wa mbegu bora za ng’ombe wa kisasa.