Wizara ya Fedha kuwajibika bajeti kuu 2022/23
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba, ameziagiza idara na vitengo vya Wizara hiyo kuhakikisha zinatimiza wajibu wake kwa ufanisi ili kuyafikia matarajio makubwa ya wananchi kutokana na mambo ambayo Serikali imejipambanua kuyatekeleza kwa mwaka wa fedha 2022/23.