Waandishi wa Habari Dodoma wasaidia Wanafunzi
Chama cha waandishi wa Habari Wanawake Mkoa wa Dodoma (DWJ), kimerejesha matumaini ya wanafunzi wawili waliokata tamaa ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano kutokana na kushindwa kumudu mahitaji mbalimbali ya shule.