Ujenzi wa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Bwa. Kaspar Mmuya amepongeza maendeleo ya ujenzi wa ofisi za msajili wa vyama vya siasa nchini zinazojengwa eneo la Kilimani Jijini Dodoma zitakazogharimu zaidi ya shilingi bilioni 20.