'Serikali inatambua mchango wa sekta binafsi'
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako, ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inathamini na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Sekta Binafsi katika ukuaji wa ajira na uchumi nchini.