Maharage ya Soya Mbeya yainuliwa
Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Anthony Mavunde ameupongeza mkoa wa Mbeya chini ya uongozi wa Mkuu wa mkoa huo Juma Homera, kwa kuchukua hatua ya uanzishwaji wa mashamba makubwa (block farms) ambayo ni maalum kwa ajili ya kilimo cha Maharage ya Soya.