Mwalimu afa kwa moto, funguo za nyumba zakutwa nje
Mwalimu wa shule ya sekondari ya Morogoro Daudi Senyagwa, amefariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kutekea kwa moto akiwa amelala ndani usiku wa kuamkia leo Juni 15, 2022 katika mtaa wa Seminari, Kata ya Kingolwila Manispaa ya Morogoro.