Mtama ulitambulishwa mkoani Singida miaka mitano iliyopita. Ni zao lililoiweka Singida katika orodha ya wazalishaji wakuu ambao wengi ni wakulima wadogo wadogo, wanawake. Kwa sasa mtama unaingizia halmashauri ya Singida zaidi ya 70% ya mapato yake.
Pamoja na kuwa na matumizi ya chakula mbalimbali, mtama unatumika pia kama dawa asilia inayoweza kupunguza makali na hata kuwa kama tiba ya magonjwa kama kisukari, presha na ongezeko la mafuta katika mwili.
Lilikuwa ni jambo la kushangaza jinsi mkulima huyu alivyofanikiwa kuzalisha ndizi Singida, mkoa ambao ardhi yake ni ya ukame hivyo zao kama ndizi haliwezi kustahimili. Alichotufundisha mkulima huyu ni kwamba penye nia pana njia