Tanzania ina vijiji endelevu vitatu ambavyo vipo chini ya mradi wa kuviwezesha kufanya majaribio ya kutathmini, kutumia mbinu za ubunifu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na uwepo wa uhakika wa chakula. Kijiji kimojawapo ni Chololo, Dodoma
Shuguli nyingi zinazofanyika ndani ya Chololo kijiji endelevu ni zile zinazozingatia kulinda na kuhifadhi maliasili ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hivyo inawalazimu wanajamii kujifunza mbinu mbadala za kuwanufaisha na kuwaendeleza
Wazalishaj wa mafuta ya alizeti kutoka Chamwino wamepata tenda ya miezi 6 ya kuuza lita 2000 za mafuta kwa kampuni ya global source organic. Hili ni dili kubwa wa wakulima wadogo wadogo kama hawa