Jumatatu , 31st Oct , 2022

Zaidi ya vijana 900 wanaofanya biashara ya chipsi wametakiwa kutumia fursa ambayo wamewezeshwa na kupewa mafunzo yaliyolenga utunzaji wa kumbukumbu na hesabu, huduma kwa wateja na ukuzaji wa mtaji, kama sehemu ya mpango wa ujumuishaji wa vijana kiuchumi wa Coca-Cola Kwanza.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Prof.Joyce Ndalichako kushoto akiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Coca cola kwanza Unguu sulay

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Prof.Joyce Ndalichako wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo pamoja na kukabidhi vifaa kwa wafanyabiashara vijana 900 waliojitokeza.

Pamoja na mambo mengine amezitaka taasisi na sekta binafsi nchini kuunga mkono juhudi za serikali katika Uwezeshaji wa makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kwa kuendelea kubuni njia mbalimbali za kutengeneza fursa za ajira nchini.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa Coca-Cola Kwanza, Unguu Suley amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuthamini ushirikiano na serikali na kuhakikisha uendelevu wa biashara kwa wajasiriamali wachanga nchini na kuweka wazi kuwa utoaji wa elimu kwa jamii ndio ukombozi katika nyanja muhimu za kiuchumi hali inayochagiza maendeleo ya jamii husika

Kmpuni hiyo imeweka wazi kuwa uwezashwaji huo ni muendelezo wa kuboresha utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara nchini ambapo amebainisha kwamba kampuni hiyo imetoa majiko ya gesi 300, mitungi ya gesi ya kilo 15, makabati, meza, aproni pamoja na kofia na kuwataka vijana waliopata vifaa hivyo kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuongeza thamani ya biashara zao