
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy aidha alitia saini amri inayoanzisha mchakato wa kuiondoa nchi yake kwenye Mkataba wa Ottawa wa kupambana na mabomu ya ardhini, kulingana na waraka uliochapishwa kwenye tovuti ya rais.
"Kwa hili natoa amri ... kutekeleza uamuzi wa Baraza la Usalama na Ulinzi la Kitaifa la Ukraine la tarehe 29 Juni 2025 kuhusu kujiondoa kwa Ukraine" kwenye mkataba wa Ottawa, Zelenskyy alisema. #EastAfricaRadio