Ijumaa , 22nd Jul , 2022

Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia nchini kumepeleka baadhi ya wafanyabishara wasio waaminifu jijini Mwanza kuzalisha mafuta katika mazingira machafu na kuwauzia wananchi.

Baadhi ya ndoo zinazohifadhia mafuta machafu

EATV imefika katika eneo la Igogo wilayani Nyamagana, katika kiwanda cha Voil ambacho mamlaka husika zilisitisha uzalishaji wa mafuta katika kiwanda hicho miaka mingi iliyopita kutokana na changamoto ya uendeshaji wake lakini leo hii kinazalisha mafuta kinyemela katika mazingira hatarishi.

Aidha wananchi wakazi wa eneo hilo ambao ndiyo watumiaji wa mafuta hayo wamelaani uzalishaji wa mafuta hayo kuendelea na kusema wengi wanaugua magonjwa ya moyo kutokana na kutumia mafuta mabaya ambayo hajathibitishwa.

Dickson ni mtendaji wa Kata ya Igogo na Ramadhan Mahela ni diwani wa Kata hiyo, wamesema wanafahamu kuhusu kiwanda hicho kutengeneza mafuta machafu huku wakitaka mamlaka zinazohusika kuchukua hatua.