Jumapili , 11th Dec , 2022

Zaidi ya Wapanda Mlima 200 wakiwemo mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani leo wamepokelewa katika Lango la Marangu ikiwa ni baada ya kukamilisha zoezi la kusimika Bendera ya Taifa katika kilele cha Mlima mrefu zaidi barani Afrika Kilimanjaro .

Zoezi hilo la kusimika Bendera liliongozwa na Brigedia Jenerali Salumu Mnumbe ikiwa na lengo la kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru wa Nchi yetu Tanzania na kuhitimishwa na Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu.

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika kusherehekea Uhuru wa nchi yetu limekuwa likiandaa zoezi hili Kila mwaka kwa kushirikiana na wadau, Mashirika ya Kiserikali, na binafsi kupandisha wageni katika kilele hicho cha Mlima Kilimanjaro zoezi ambalo huongozwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).