Mmachinga wafurahia ahueni waomba kuongezwa muda

Jumanne , 15th Sep , 2020

Wafanyabiashara wadogo wadogo ambao walinufaika na vitambulisho vilivyotolewa na serikali kwa ajili ya kuwasaidia kutambulika rasmi katika ulingo wa biashara wametaka wale waliofanikiwa kupitia mkakati huo na kukua kuwaachia wengine ili waweze kunufaika.

Wakizungumza na EATV wafanyabiashara hao wamesema kuwa vitambulisho hivyo vimekuwa na manuifaa makubwa katika uendelezaji wa biashara zao ikiwemo kupunguza usumbufu ambao waliokuwa wanaupata kutoka kwa mgambo wa Jiji ikiwa ni pamoja na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi hivyo kutaka waliionufaika na kupanda ngazi kibiashara kutoa nafasi kwa wengine kuweza kupata vitambulishi hivyo.

Wamesema licha ya mafanikio waliyopata hadi sasa suala la wateja bado limekuwa chachu kwa maendeleo kutokana na ongezeko la wafanyabiashara wa aina moja za biashara katika sehemu moja hivyo kuomba kuboreshewa kwa kupatiwa maeneo kulingana na aina za biashara pamoja na kupatiwa mafunzo zaidi ya namna ya kujiendeleza na kuwafikia wateja kulingana na mahitaji ya mlaji.

"Vimetusaidia sana kwakweli adha tuliyokuwa tunapata mwanzo hatupati tena, ila tunaombi vitambulisho viwe vya mwaka mmoja sio miezi sita kama ilivyosasa na wengine wanaopata wawe waaminifu" alisema Mustapha Mmoja wa wafanyabiashara