Tigo yatoa zaidi ya Mil 20 kwa mawakala kinara

Jumatano , 8th Jan , 2020

Washindi wawili wa promosheni ya wakala kinara, kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, wamejinyakulia zawadi zao kila mmoja, akiwemo Hajira Fadhili, ambaye ni mkazi wa Ilala, Jiji la Dar es Salaam, aliyejinyakulia kiasi cha Shilingi milioni 20.

Mkuu wa Kitengo cha Tigopesa, Angelica Pesha, katikati akiwa na washindi wa promosheni ya wakala kinara.

Akitangaza zawadi hizo kwa washindi hao wa Kitaifa leo Januari 8, 2019, Mkuu wa Kitengo cha Tigopesa, Angelica Pesha, amesema kuwa mshindi wa pili ni Suleiman Hussein, aliyejinyakulia kitita cha Shilingi milioni 10, ambaye ni mkazi wa Zanzibar.

"Zaidi ya Shilingi milioni 50 zimeshindaniwa, ambapo mshindi wa kanda wa kwanza alipata Shilingi milioni tatu, wa pili alipatiwa Shilingi milioni 2" amesema Angelica.