Alhamisi , 30th Jun , 2016

Abiria wanaotumia usafiri wa treni kati ya Mpanda, Tabora hadi Dar es Salaam, wamelalamikia ,tatizo la kukosekana kwa nafasi kutokana na uchache wa mabehewa katika treni hiyo.

Abiria hao wamemwambia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Kadogosa Masanja, alietembelea vituo vya treni hiyo katika mikoa ya Tabora na Katavi, kuwa wanapata usumbufu mkubwa kwa kukosa nafasi katika treni.

Akielezea sababu ya kukosekana kwa nafasi hizo Meneja wa Shirika la Reli Kanda ya Tabora,Fred Masangwa, amesema kuwa kawaida kipindi hiki cha mavuno kuna watu wengi wanaosafiri nakusababisha kukosa nafasi.

Kwa upande wake Mkurugenzi huyo wa shirika la reli nchini Kadogosa Masanja amesema ili kuondokana na tatizo hilo wataongeza idadi ya mabehewa kutoka sita yaliyopo hivi sasa hadi kufikia mabehewa nane.