Jumatano , 24th Aug , 2022

Dickson Beno Mwenda (37) ambaye ni Afisa mipango miji wa Halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi  anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka binti mdogo mwenye umri wa miaka 15 ndani ya gari

Kamanda wa Polisi Katavi Ally Makame amesema mtuhumiwa huyo alikabidhiwa watoto wawili na mama yao ambaye walikuwa wanakunywa pombe pamoja bar awapeleke nyumbani ndipo akiwa njiani alitekeleza unyama huo 

Polisi wamesema katika mahojiano ya awali mtuhumiwa amekiri kosa na leo hii baada ya uchunguzi kukamilika anafikishwa mahakamani

Pia Jeshi la Polisi limefanikiwa kumnasa na kumkuta na mali za wizi John Gaudensi ambaye alivunja nyumbani kwa mwalimu Kenani Kasekwa ambaye ni karani wa sensa na kuiba Kishkwambi cha sensa, radio, simu na pesa taslimu sh 760,000 vyenye jumla ya thamani ya sh milioni moja laki tatu na elfu ishirini.