Jumatatu , 31st Aug , 2015

Wananchi wa eneo la Misugusugu Wilayani Kibaha Mkoani Pwani hii leo wamefunga barabara baada ya Wanafunzi wawili kugongwa na gari la Jeshi la Polisi na kupelekea kifo cha Mwanafunzi Mmoja

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Jaffary Mohammed

Akiongea na East Africa Radio Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Jaffary Mohammed amesema baada ya tukio hilo Wananchi walifunga barabara kutokana na hasira ya tukio lakini jeshi la Polisi limetuliza hali na linamshikilia Dereva wa gari hilo kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda Jaffary ameongeza kuwa katika tukio hilo Mwanafunzi aliyejeruhiwa amelazwa katika hospitali ya Tumbi na mwili wa marehemu upo mochwari katika hospitali hiyo.

Aidha Jaffari ameongeza kuwa kwa sasa hali ya kiusalama imetulia baada ya jeshi la polisi kutuliza hali iliyojitokeza huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi na badala yale wafate sheria.

Katika hatua nyingine amewataka madereva wafuate sheria za barabarani kwa kufuata alama zilizowekwa pamoja na kupunguza mwendo katika maeneo ya watu ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.