Jumapili , 11th Jan , 2026

Serikali ya DRC inasema inafuatilia kwa karibu kinachotokea kwa raia wake nchini Burundi, na inafanya jitihada za kuwapelekea chakula, dawa na mahitaji mengine muhimu.

Wakimbizi zaidi ya 50 waliokimbia machafuko katika nchi yao ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamepoteza maisha wakiwa kambini, katika nchi jirani ya Burundi.

Shirika la Umoja wa Mataifa, linaloshughulikia wakimbizi limesema watu 53 wamefariki dunia, 25 yao wakifariki kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu huku wengine wakifariki baada ya kuambukizwa ugonjwa wa anemia na changamato za utapiamlo.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa unashirikiana na Wizara ya afya nchini Burundi na washirika wake ili kuchunguza zaidi kuhusu vifo hivyo na kuzuia maambukizi mengine yanayoweza kutokea.

Serikali ya DRC inasema inafuatilia kwa karibu kinachotokea kwa raia wake nchini Burundi, na inafanya jitihada za kuwapelekea chakula, dawa na mahitaji mengine muhimu.

Hali ya usalama Mashariki mwa DRC hasa Kivu Kusini, imeendelea kuwa mbaya tangu mwezi Desemba, baada ya waasi wa M23 kuuchukua mji wa Uvira na kusababisha Wakongomani zaidi ya 100,000 kukimbilia nchini Burundi.