
Watu watano wanaripotiwa kuuawa, akiwemo afisa mmoja wa polisi na mshukiwa wa mauaji aliyekuwa na silaha, huku mtu mmoja akijeruhiwa, kufuatia ufyatuaji risasi katikati ya mtaa wa Manhattan, jijini New York.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha polisi, mtuhumiwa wa mauaji hayo akitambulika kama Shane T., 27 ametumia bunduki aina na M4 na alikufa baada ya kujipiga risasi mwenyewe. Afisa wa polisi aliyeuawa ametambuliwa kama Didarul Islam, aliyezaliwa nchini Bangladesh.
Meya wa jiji hilo, Eric Adams, ameandika kupitia mtandao wa X kwamba bado wanachunguza chanzo cha tukio hilo.
Majina ya wahanga wengine wa mauaji hayo hawajatajwa, lakini eneo yalikofanyika ni makao makuu ya mashirika makubwa ya kibiashara, yakiwemo ya Colgate Palmolive na KPMG.
Matukio ya mashambulizi ya ovyo ovyo yamekuwa ni jambo la kawaida nchini Marekani, kutokana na sheria kuruhusu watu kutembea na silaha wapendavyo.