Jumatatu , 22nd Dec , 2025

Mwili wa marehemu, Patric Francis, umekutwa unaning'inia ndani ya banda la mbuzi nyumbani kwao, alipokuwa akiishi na wazaazi wake.

Patrick Francis (35) mkazi wa kijiji cha mapea, wilayani Babati mkoani Manyara, amefariki dunia baada ya kujinyonga ndani ya banda la mbuzi, huku chanzo cha tukio hilo kikiwa hakijafahamika.

Mwili wa marehemu, Patric Francis, umekutwa unaning'inia ndani ya banda la mbuzi nyumbani kwao, alipokuwa akiishi na wazaazi wake.

Jeshi la Polisi wilaya ya Babati mkoani Manyara, limefika eneo la tukio na kuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi kutaka kubaini chanzo cha kifo hicho uchunguzi unaendelea.

Eatv tumezungumza na mwenyekiti wa kijiji cha mapea ambaye amekiri kutokea tukio hilo huku mama mzazi wa marehemu huyo akidai kuna siku mwanaye alimwomba kamba ya kujinyonga na kumkataza asifanye hivyo.