Jumatatu , 5th Dec , 2022

Mwenendo wa soko la hisa la Dar es salaam kwa wiki iliyoishia desemba 2 umeonesha kupungua kwa thamani ya hati fungani zilizoorodheshwa sokoni kwa shilingi 5 bilioni kutoka 16.80 trilioni kwa wiki iliyoishia novemba 25,2022.

Katika upande wa ukwasi sokoni hapo upande wa hisa umeongezeka kwa shilingi bilioni 4 ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.7 kwa mujibu wa ripoti iliyowasilishwa na meneja uendelezaji biashara Leonald Kameta ambaye amebainisha mchango na ushiriki mkubwa kwa kampuni za ndani umezidi kuimarika

“Kwa hali ilivyo sasa kwenye ukubwa wa mtaji sokoni hapo umeongezeka hasa kwa wiki iliyoishia desemba 2,2022 kutokana na kuongezeka kwa bei za makampuni kadhaa za ndani”amesema Leonald

Kuhusu uwekezaji kwenye hati fungani zile za miaka 20 zimeonekana kupendwa zaidi kutokana malengo ya wawekezaji.