Vifaa hivyo vilivyokamatwa vinatajwa kuwa thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 9, ambapo Kamanda wa Polisi mkoani humo, Simon Marwa amesema kuwa alipokea taarifa kutoka kwa wasamalia wema ambao walibainisha juu ya kuwepo kwa watuhumiwa hao.
"Kwa ujumla tumewakamata watu hawa wawili walioiba mali ya Shirika la Umeme ambayo ilikabidhiwa kwa Mkandarasi aliyekuwa anashughulikia anaitwa NAPSI ambaye alikuwa anaendelea na miradi ya umeme ndipo wezi hawa walifika kuiba", amesema Kamanda Simon Marwa.
Aidha Kamanda huyo amesema Jeshi la Polisi linamshikilia Kassim Zuberi kwa makosa ya kukutwa na silaha ya moto ambayo aliitengeneza kwa njia ya jadi, bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mamlaka hiyo.