
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, Mratibu Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto, Hamis Shabani Dawa amethibitisha kuwa tukio hilo limetokea leo Augost 04 2025 majira ya saa kumi na mbili alfajiri na kuongeza kuwa chanzo cha tukio hilo bado hakijabainika.
Aidha, Kamanda Dawa amewasihi wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa wakati kabla ya moto haujaleta madhara makubwa.
Kwa upande wa mmiliki wa karakana hiyo, Bwana Phinias Aloyce amesema vitu vilivyoteketea vinakadiriliwa kuwa na thamani ya shilingi milioni nane.