
Fedha bandia zilizokamatwa
Tukio hilo limetokea Novemba 4, 2022, kwa wakala wa fedha Ndaleta usiku wa saa 2:00 kijijini hapo ambapo mtuhumiwa alitaka kuweka fedha hizo kwenye akaunti yake ya simu.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Ndaleta Ijumaa Bakari, akizungumzia tukio hilo alisema mtuhumiwa alifikishwa ofisini kwake na wakala huyo wa fedha jina limehifadhiwa wakiwa na fedha hizo bandia na baada ya kuulizwa alisema kuwa ni zake naye alipewa.
Alisema baada ya kukiri aliagiza mtuhumiwa afikishwe kituo cha Polisi Kibaya kwa hatua zaidi za kisheria
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Manyara RPC George Katabazi amethibitisha tukio hilo na kuwataka wananchi kuwa makini kutambua fedha bandia na kutoa taarifa Polisi.