
Waokoaji walisherehekea baada ya kumpata mwanamke huyo akiwa hai wiki moja kupita tangu jengo hilo kuporomoka, ambapo mwanamke huyo alionekana kudhoofika mwili lakini hana majeraha.
Tukio hilo linafuatiwa na tukio la jumanne ambapo mtoto wa miezi sita aliokolewa akiwa hai kutoka kwenye vifusi, na kisha sungura tisa kuokolewa wakiwa hai jumatano. Watu 33 wamethibitishwa kufa hadi sasa.