Jumanne , 28th Feb , 2023

Mwanamke mmoja  aliyejiwakilisha mwenyewe mahakamani kwa kutumia sheria ya kandarasi ya miaka 80 amelishinda Shirika la Ndege la Uingereza (British Airlines) mfululizo kuhusu  fidia ya vocha za ndege.

Mnamo Januari 2020, Jennie Barber alikata tiketi mbili za ndege za kurudi Japan zikiondoka mwezi  Mei , lakini baadaye ndege hizo ziliondolewa kutokana na vizuizi vya Covid. Shirika hilo la dnege  ilitoa marejesho kwa njia ya vocha za usafiri lakini Bi Barber alitaka pesa zake zirejeshwe na  Shirika la ndege lilikataa.

Akijiwakilisha mwenyewe, Bi Barber alilipeleka shirika hilo  mahakamani na kushinda marejesho yake kamili. Mwanamama huyo emenukuliwa akisema kwamba  "Kama upo. mtu wa kawaida, ambaye si mtaalamu wa sheria, kwenda mahakamani kupambana  na mtu kama British Airways inatisha ‘’

Hata hivyo, Bi Barber, ambaye alisomea sheria ya kiwango cha A, aliweza kuishinda kampuni hiyo kubwa ya ndege mahakamani kwa kutumia Sheria ya Marekebisho ya Sheria  ya mwaka 1943.