Jumatatu , 22nd Mei , 2023

Takribani siku saba zimepita toka Jeshi la Polisi Mkoani Manyara kuripoti kukamata watu wawili wakiwa na mali za wizi ikiwemo fedha zaidi ya milioni 20 pamoja na simu 27 za mkononi, tayari polisi wamemshampata mfanyabiashara aliyeibiwa fedha hizo.

Mfanyabiashara aliyeibiwa milioni 20

Mfanyabaiashara huyo ambaye aliibiwa milioni 20 amelishukuru Jeshi la Polisi huku akiwataka wafanyabiashara wenzake kuacha tabia ya kuajiri walinzi wasio na anuani za makampuni ya ulinzi pamoja na kuacha tabia ya kuyaamini makabati ya kuhifadhia fedha.

Kupitia tukio hilo kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara George Katabazi, amewataka wananchi kuendelea kuliamini jeshi la polisi na kutoa ushirikiano katika matukio mbalimbali ya kiuhalifu.