Jumatatu , 11th Oct , 2021

Watu watatu wamefariki dunia akiwemo mama mmoja mfanyakazi wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma ambaye siku ya jana amepokea barua ya kustaafu na leo Oktoba 11, 2021, alikuwa anaenda kuwaaga wenzake baada ya bajaji waliyokuwa wamepanda kugongana na gari la JWTZ, Kata ya Mfaranyaki, Songea.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Joseph Konyo

Akielezea tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Joseph Konyo, amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:30 asubuhi ambapo gari la Jeshi lilikuwa linatokea mjini likiwa limepakia wafanyakazi liligongana uso kwa uso na bajaji ambayo ilikuwa inaelekea mjini na kusababisha vifo hivyo na majeruhi mmoja.