Jumamosi , 19th Jan , 2019

Licha ya kutangazwa kuondolewa kwenye nafasi yake na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'anzi ameendelea kufanya majukumu yake kama kamanda wa Mkoa wa huo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola.

Jana kupitia Mkutano wake na waandishi wa habari RPC Ng'anzi alitangaza jeshi lake mkoani Arusha kuwakamata baadhi ya watuhumiwa kumiliki mitambo ya kujengea fedha bandia, hali ambayo imezua sintofahamu hasa kwenye mitandao ya kijamii.

"Huyu mtuhumiwa wa kwanza aliwapeleka askari wetu nyumbani kwake eneo la Daraja Mbili ambako zilikutwa fedha bandia za mataifa mbalimbali," amesema Ng'anzi.

Waziri Kangi Lugola alitoa uamuzi huo akiwa Jijini Dodoma, ambapo ametengua uteuzi wa makamanda wa polisi wa mikoa mitatu akiwemo Salum Hamduni aliyekuwa Ilala, Emmanuel Lukula (Temeke) kwa kosa la kushindwa kusimamia mianya ya rushwa na utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa.

www.eatv.tv ilijaribu kumtafuta Waziri Lugola kwa njia ya simu yake mkononi lakini simu iliita bila kupokelewa.