Jumapili , 24th Mar , 2024

Basi la Shule ya sekondari Kemebos iliyopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, lenye namba za usajili T 770 DSQ limepata ajali na kuua mwanafunzi mmoja na kujeruhi wengine sita katika Kata ya Kimwani wilayani Muleba mkoani Kagera, huku chanzo cha ajali kikitajwa kuwa ni mwendokasi wa dereva

Basi lililopata ajali

ambaye alishindwa kukata kona.

Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga, amesema kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa nane za usiku wakati likisafirisha wanafunzi kutoka Bukoba kuelekea mkoani Geita likiwa na jumla ya wanafunzi 35

Dkt. Nyamahanga amesema kuwa Mwanafunzi  huyo ni wa kidato cha tano aliyejulikana kwa jina la Frank Matage mwenye umri wa miaka 17 wa shule ya Sekondari Kemibos iliyoko manispaa ya Bukoba huku majeruhi hao sita wote wamelazwa katika Hospital ya Rufaa ya mkoa