Jumatano , 4th Jun , 2025

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limethibitisha kumshikilia mwanamke anayefahamika kwa jina la Zulpha Mathew Timamu (26) mkazi wa Kata ya Tandika Wilaya ya Mtwara kwa tuhuma za Mauaji ya Kichanga chenye jinsia ya kiume muda mchache baada ya kujifungua, tukio ambalo lilitokea tarehe 02/06/25

Mwanamke huyo anadaiwa kufanya tukio hilo katika maeneo ya Tandika kwenye nyumba anayoishi ambapo Majirani walisikia sauti ya kichanga ikitoka kwenye nyumba hiyo na muda mchache hawakuisikia tena ndipo walipopata wasiwasi na kutoa taarifa Polisi

Chanzo cha tukio hilo ni baada ya mtuhumiwa kuona atazidiwa na majukumu ya kulea mtoto kwa kuwa alikuwa ana mtoto mwingine mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu ambaye bado ananyonya

Taarifa ya Polisi imesema kuwa uchunguzi wa awali umeonesha kuwa mtuhumiwa alijifungua salama na mtoto alikuwa hai lakini alikichukua kichanga hicho na kukiweka kwenye ndoo ndogo yenye ujazo wa lita kumi kisha kufunika ndoo kitendo kilichofanya akose hewa na kufariki #EastAfricaTV