Jumatano , 19th Jan , 2022

Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe linamshikilia Shukrani Kamwela (16), mkazi wa Ileje mkoani Songwe kwa tuhuma za kumuua kwa kumchoma na kisu mke wake aitwaye Subira Kibona (16) aliyekuwa ni mjamzito na kisha mwili wake kuuchoma moto.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe, Janeth Magomi

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe, Janeth Magomi, amesema kuwa walipokea taarifa za mwanamke huyo aliyepotea tangu Januari 13, 2022.

Kamanda magomi amesema baada ya wananchi kuamua kumtafuta mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa umetupwa porini kwenye korongo.