Migomba
Taarifa zimeeleza kuwa Otieno, alitekeleza mauaji hayo ya kinyama wiki tatu zilizopita, baada ya rafiki yake huyo kuwasili nyumbani kwake alimfukuza mke wake na kumtaka akalale chumba kingine na kisha yeye alale na rafiki yake na ndipo alipotekeleza unyama huo.
Polisi wamesema tukio hilo lilitokea nyumbani kwa mshukiwa katika kijiji cha Nyamaraga, kaunti ndogo ya Suna Magharibi, Migori.
Aidha imeelezwa kuwa mwanaume huyo baada ya kumuua rafiki yake alipatwa na mfadhaiko na alikuwa hatoki ndani hadi Machi 4, 2022, ndipo alipoamua kwenda kuvua samaki, nafasi ambayo mke wake aliitumia kupiga simu polisi na kutoa taarifa juu ya utata ya wapi alipo rafiki wa mume wake.





.jpg?itok=5cvL0YaP)