Ofisa Habari Mahusiano ya Umma wa Chama cha Albino Tanzania Josephat Torner (kushoto), akizungumza
Akizungumza, afisa habari wa cha hicho Josephat Tona amesema hali hiyo inatokana na uhaba wa madaktari bingwa wa magonjwa ya ngozi,umbali wa hospitali za magonjwa ya saratani ya ngozi na gharama kubwa ya mafuta maalumu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.
Tona ameongeza kuwa wanaitaka serekali kuongeza madaktari wa magonjwa ya ngozi kufuatia uchache wa madakatari hao ukilinganishwa na ukubwa wa nchi.
Kwa upande wao watu wenye ulemavu wa ngozi na wasioona pamoja na kuziomba taasisi mbalimbali kuwasaidia kupata mahitaji muhimu kwao ,pia wameiomba serikali kuweka fungu maalumu kwa walemavu wa ngozi walioathirika na saratani ya ngozi , ili wapate matibabu ili kuondokana na vifo kwa kukosa huduma mapema.
Naye katibu mkuu wa chama cha albino Tanzania Ziada Nsembo amesema pamoja na madaktari kuwa wachache waliokuwepo katika mikoa wapewe usafiri ili kuweza kuwafikia wenye ulemavu wa ngozi waliokwisha anza kuathirika na saratani kwa urahisi ili kupunguza vifo .





