Jumatatu , 21st Sep , 2015

Serikali kupita Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema kuwa asilimia 80 ya madawa ya binadamu yanayotumika hapa nchini yanatoka nje ya nchini kutoka na ukosefu wa uwekezaji mdogo wa viwanda vya dawa nchini.

Katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii Dokta Donann Mmbando.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Dr. Donann Mmbando leo jijini Dar es salaam katika mkutano wa wadau wa sekta ya Madawa walipokutana kujadili Miongozo na kanuni mpya za pamoja za uzalishaji na matumizi ya dawa katika jumuiya ya Afrika mashariki.

Dr Mbando amesema kuwa hata hivyo serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri ili kuwezesha wawekezaji kuja nchini kujenga viwanda vingi vya madawa ya binadamu kufidia pengo lililopo hapa nchini.

Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA, Hiiti Sillo amesema Jumuiya Afrika mashariki ndio jumuiya ya kwanza Afrika kutumia miongoni mwa kanuni za pamoja za kudhibiti madawa zinazokubalika na shirika la Afya Duniani.