
Farid Mussa akiwa na wakala wake baada ya kutua hapo Hispania jana usiku
Akizungumza kutoka Madrid, Hispania, Farid amesema leo ndiyo atajua ratiba nzima ya mazoezi.
Farid atakuwa nchini humo kwa muda wa mwezi mmoja akifanya majaribio klabu za Union Deportiva Las Palmas, maarufu kama Las Palmas yenye maskani yake Las Palmas de Gran Canaria na Athletic ya Bilbao.
Farid amewasili Hispania akitoka kuichezea klabu yake, Azam FC katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Esperance walioshinda 3-0 mjini Tunis Jumanne.