
Farid Mussa akiwa Makao Makuu ya Deportivo Tenerife, Uwanja wa Heliodoro Rodriguez Lopez,visiwa vya Canary Hispania
Wakala wa Farid, John Sorzano raia wa Venezuela aliyeishi sana nchini England amesema, ameamua mchezaji huyo aanzie timu ya Daraja la Kwanza Hispania ili kupata nafasi ya kucheza na kuinuka haraka, tofauti na mpango wa awali ambapo walitarajia angeznia timu mojawapo ya La Liga kati ya Las Palmas na Athletic ya Bilbao.
Farid atafanya majaribio hayo na kukaa huko kwa takribani wiki tatu na anatarajia kurejea nchini Mei 19 mwaka huu, ikiwa na maana kuwa atakosa mechi zote za Azam FC zilizobakia za msimu huu.
Farid alikwenda Hispania Alhamisi akitoka kuichezea klabu yake, Azam FC katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Esperance walioshinda 3-0 mjini Tunis Jumanne.