Ijumaa , 14th Feb , 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amesema kuwa wananchi wengi wanapenda kuingia kwenye mitandao ya kijamii na kufuatilia mambo ya watu, badala hata ya kutumia muda huo kuweka post itakayotangaza utalii wa nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Makonda ameyabainisha hayo leo Februari 14, 2020, wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tambaza, alipofika hapo kwa ajili uhamasishaji wa zoezi la uandikishwaji wa wananchi katika daftari la wapiga kura.

"Katika eneo pekee ambalo Watanzania tumefanikiwa ni katika umbea kwa asilimia 99.9, ukiangalia Instagram yako, Twitter na Facebook yako hata kupost tu aina ya mnyama mmoja na tabia zake hauwezi ila umbea una forward masaa 24, halafu mwisho wa siku unataka bweni umechangia nini wewe" amesema RC Makonda.

Zoezi la uandikishwaji wa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura, umeanza leo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, zoezi ambalo litadumu kwa muda wa siku sita.