Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda Wankyo amesema tukio hilo lilitokea Januari 18 majira ya saa 12 jioni na kutaja kuwa Askari Yusuph alikua akitumikia kituo c na alikua akiishi maeneo ya Picha ya ndege lakini siku ya tukio alienda Kongowe eneo ambalo anaendelea na ujenzi na ndipo alipokutwa amejinyonga na kamba.
Askari huyo mwenye umri wa miaka (52) aliyekuwa anafanya kazi katika kituo cha Polisi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani namba 6472 amekutwa amejinyonga hadi kufariki dunia katika nyumba yake anayoijenga katika maeneo ya miembe saba.
Kamanda alibainisha kwamba uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea wakati taratibu za kumsafirisha marehemu kwenda kwao Lindi kwa maziko zikiendelea.
Aidha kwa upande wa Msaidizi wa balozi kwenye eneo hilo Imelda Kitosi alisema akiwa nyumbani alipigiwa simu kuwa kuna tukio la mtu kujinyonga ndipo akaenda kushuhudia akiwa na baadhi ya majirani na alipofika alielezwa na wazazi wa watoto waliokuwa na karibu ya eneo hilo kuwa kuna watoto waliokuwa wanacheza kombolela nje ya nyumba hiyo ambao walisema walisikia mtu anajipiga ndani ya nyumba na walipochungulia wakamkuta tayari yupo chini akiwa na kamba shingoni na walikimbia kwenda kutoa taarifa.