Jumamosi , 30th Dec , 2017

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kituo cha Nansio wilayani Ukerewe, Mkoani Mwanza  John Kalongola amejinyonga kwa kipande cha chandarua nyumbani kwake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema mwili wa askari huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe.

Amesema baada ya uchunguzi na utaratibu kukamilika mwili utasafirishwa kwa mazishi mkoani Iringa ambapo amesema mwili huo ulibainika baada ya harufu kutoka ndani ya nyumba yake na mlango ulipovunjwa ulikutwa ukining’inia.

 Mwili wa askari huo uligunduliwa jana Ijumaa Disemba 29, 2017.na kusema kipande cha chandarua kilifungwa juu ya dari