Ijumaa , 11th Sep , 2020

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia chama hicho saed Kubenea, aliyekuwa amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kuingia nchini kinyume na Sheria ya Uhamiaji, atazungumza siku za hivi karibuni.

Saed Kubenea

Taarifa hiyo imetolewa hii leo Septemba 11, 2020, na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa chama hicho, Janeth Rithe, muda mfupi tu tangu mgombea Ubunge huyo kupata dhamana baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria katika kesi inayomkabili.

Taarifa hiyo pia imewapongeza mawakili waliofanikisha hatua ya Kubenea kupata dhamana hiyo, huku wakiwasihi wanachama wa chama hicho kufuatilia ratiba ya mikutano ya kampeni ili waweze kusikiliza sera na ahadi zilizomo kwenye ilani ya chama hicho.

"Aidha Ndugu Saed Kubenea, anatarajia kuzungumza na vyombo vya habari katika siku za hivi karibuni juu ya suala hili", imeeleza taarifa hiyo.