Jumatano , 20th Jul , 2016

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki, amesema wilaya ya Bagamoyo inaongoza kwa kuwa na taarifa chafu katika mkoa wa Pwani.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki

Waziri Kairuki amesema hayo jana katika ziara yake ya siku moja ya kutembelea na kuzungumza na watumishi wa Umma ambapo amesema wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya tatu zinazoongoza kwa watumishi hewa mkoani Pwani.

Mhe Kairuki amesema kuwa watumishi 2206 wenye makosa mbalimbali ya kimfumo kwenye malipo yao ambapo amesema kati ya watumishi hao watumishi wasiokuwa na taarifa za elimu ni2173 na wenye miaka zaidi ya 60 ni 14 na 21 wanakosa mfumo wa malipo ya mshahara.

Amesema kuwa endapo mafisa Utumishi wakiwa hawajakamilisha uhakiki kwa watumishi wengine wa umma ifikapo Agosti mwaka huu watasababisha watumishi hao kunyimwa mishahara yao.

Aidha Waziri Kairuki amesema kuwa wapo watumishi wanaolipwa mishahara na taarifa zao za kimsingi zikiwa na utata ikiiwemo kutobainishwa kwa taarifa za elimu za benki barua za ajira.