Jumapili , 4th Sep , 2022

Kamishna wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA), Dkt. Peter Mfisi, amesema kwamba dawa ya kulevya inayoongoza kwa kutumiwa zaidi hapa nchini ni bangi ikifuatiwa heroin.

Bangi

Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni wakati akizungumza kwenye #EATVSAA1 ya East Africa TV, na kusema sehemu ya heroin inayoingizwa hapa nchini husafirishwa na kupelekwa kwenye masoko mengine duniani ikiwemo China na Marekani.

"Dawa inayotumika zaidi hapa nchini kwetu ni bangi kama unavyojua bangi inastawi karibu kila mahali hapa nchini karibu mikoa yote inastawi, na inastawi hata kwenye udongo wa ajabu ajabu sijui kwanini, nafikiri ndiyo maana imekuwa ipo available na inatumika kwa kiwango kikubwa hapa nchini," amesema Dkt. Mfisi