BAVICHA kuzuia mkutano wa CCM Dodoma

Jumamosi , 2nd Jul , 2016

Baraza la Vijana la Chama cha Demoktasia na maendeleo nchini CHADEMA limesema litahakikisha linashirikiana na jeshi la polisi kuzuia mkutano mkuu wa Chama cha mapinduzi CCM unaotarajiwa kufanyika mjini Dodoma Julai 23 mwezi huu.

Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la CHADEMA,(BAVICHA), Julius Mwita.

Wakizungumza na waandishi wa habari leo viongozi wa BAVICHA wamesema hatua yao hiyo ina lenga kuunga mkono kauli ya serikali ya kuzuia mikutano ya kisiasa kote nchini ili kutoa nafasi kwa wananchi kufanya kazi

Viongozi hao wa BAVICHA Makamu mwenyekiti Bw. Patricia Olesosopi pamoja na Katibu mkuu wake Bw. Julius Mwita wamesema watashirikiana na vijana wa BAVICHA kuona agizo la kuzuia mikutano hiyo linatekelezwa na si vinginevyo.

Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kumkabidhi uenyekiti wa Chama hicho Rais John Pombe Magufuli kwa mujibu wa katiba yao unatarajiwa kufanyika tarehe 23 June, mwaka huu mjini Dodoma.