
Serikali mpya ya Netanyahu inatarajiwa kuapishwa mjini Jerusalem ikiwa ni miezi miwili baada ya waziri mkuu huyo mteule kushinda uchaguzi wa bunge nchini humo
Hii ni serikali ya siasa za mrengo wa kulia zaidi ambayo Israeli imewahi kuwa nayo, huku wanasiasa wa siasa kali za mrengo huo pia wakijumuishwa kwa mara ya kwanza katika serikali ya mseto